Uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki katika Ziwa Victoria

InfoNile inawakaribisha wanahabari wanawake kutoka nchi za Uganda, Kenya na Tanzania, kuwasilisha maombi ya kuandika habari za; ‘Uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki katika Ziwa Victoria’.

Habari hizo ni mfululizo wa habari zinazoangazia madhara ya uchafuzi wa mazingira unaotokana na plastiki na uvumbuzi wa ndani uliofanywa ili kukabiliana na uchafuzi huo. Mradi huu utajikita katika masuala ya  uandishi wa takwimu, ramani, usanifu  na habari za kawaida.

Wakati bidhaa za plastiki zikiwa na matumizi mengi, lakini pia zinatajwa kuwa na madhara ya kimazingira duniani. Kwa mujibu wa UNEP, zaidi ya tani 300 milioni ya uchafu unaotokana na plastiki zinazalishwa duniani kila mwaka.

Kwa sababu plastiki kwa kawaida haziozi kwa haraka, hivyo hazipotei kabisa zinapotua ardhini au majini, bali hubaki na kuendela kuwa ndogo. Tafiti zimeonyesha kuwa, kuna uwepo wa plastiki ndogondogo katika ziwa Victoria, na katika samaki ambao huishi nazo. 

Hata hivyo,  habari za uchafuzi unaotokana  na plastiki ndogo ndogo katika nchi za Maziwa Makuu Afrika, haziandikwi kwa wingi ukilinganisha na  nchi nyingine duniani.

Hivyo basi, tunatamani wawepo wanahabari watakaoandika habari za uchafuzi wa mazingira utokanao na taka za plastiki katika jamii yao na kando ya ziwa Victoria.

Kadhalika, habari zitakazoandikwa hazina budi kwenda sanjari na ‘FlipFlopi Expedition’ ambayo ni sehemu ya mradi huu’. FlipFlop Expedition ni boti ya asili iliyotengenezwa kwa kutumia taka za plastiki. Boti hii inazunguka na kufanya msafara Afrika Mashariki katika ziwa Victoria kwa ajili ya kuhamasisha kuhusu uchafuzi wa majini.  

Ufadhili huu utatolewa kwa wanahabari  wenye mitazamo tofauti ili kupata habari za uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na taka za plastiki na namna wakazi wa maeneo hayo wanavyoathiriwa na tatizo hilo. 

Tafadhali bonyeza linki hii here   kuangalia msafara wa boti hiyo na ikiwezekana bainisha habari zitakazoangazia masuala ya uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki au suluhisho

Unachotakiwa kufanya:

 1. Kuhusisha sayansi, tafiti na takwimu na uhalisia wa uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki na hatua zilizochukuliwa katika jamii yako.
 2. Kufanya uchunguzi wa kina kuhusu uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki , madhara yake kwa bioanuwai na jamii zilizo katika Ziwa Victoria AU kuonyesha suluhisho la uchafuzi huo katika Ziwa Victoria na visiwa vilivyomo ndani yake. 
 3. Kuhusisha habari yako na hadhira kitaifa na katika jamii

Maswali yanayotakiwa kujibiwa katika habari yako:

 1. Ni kwa namna gani uchafu wa plastiki unaathiri jamii? Unaathiri vipi bioanuwai?
 2. Ni kwa namna gani wakazi wa jamii ya Ziwa Victoria wanakabiliana na changamoto zinazosababishwa na uchafuzi wa taka za plastiki ziwani? Wanatumia ubunifu gani kupambana na changamoto hizo?
 3. Takwimu zipi, tafiti za kisayansi au ushahidi unaoweza kuupata ili kuthibitisha kuwa kuna tatizo hilo katika jamii hiyo? Na matokeo ya suluhisho lililochukuliwa?
 4. Ujumuishi wa Takwimu: Habari yako haina budi kuwa na mpango wa kazi wa namna ya uchambuzi wa data na kuonyesha uchafuzi wa taka za plastiki na madhara yake kwa bioanuwa na  watu wa eneo hilo.
 5. Takwimu za kijiographia ndizo zinazohitajika zaidi, kwa sababu zitatumika kutengeneza ramani na picha. Hata hivyo, jisikie huru kutumia vyanzo vingine vya habari vyenye takwimu za uhakika.

Matokeo

Matokeo ya utafiti wako, yanatakiwa kuonekana katika habari ya kina, itakayojikita katika kuonyesha madhara ya uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki katika eneo lako au kuonyesha suluhisho la kipekee au njia mbadala za matumizi makubwa ya plastiki.

Kumbuka kuwa, iwapo utapata ufadhili wa kukuwezesha kuchapisha habari yako, utapewa pia msaada wa kutengenezewa takwimu kwa njia ya picha na ramani. Habari zitakazoandaliwa, zinaweza kuchapishwa katika lugha nyingine au kutafsiriwa pia kwa lugha ya Kiingereza.

Mradi huu unafadhiliwa na taasisi ya Code for Africa kama sehemu ya Mradi wa Maji. Mwisho wa maombi ya kuwasilisha mpango kazi wa habari yako ni Februari 8, 2021. 

Infonile ni ushirikiano wa wanahabari za mazingira  wenye lengo la kuibua habari za masuala ya maji katika nchi zinazozungukwa na bonde la Mto Nile, kwa kutumia takwimu, na mitandao ya kijamii au media anuwai. 

Infonile hufanya miradi ya habari za uchunguzi na uandishi wa habari kwa njia ya data hasa katika masuala ya kina ya maji na mazingira katika ukanda wa Mto Nile. Habari za uchunguzi zilizowahi kufanyiwa kazi ni pamoja na  land grabs across the Basin, community-based solutions to wetland destruction in East Africa, and the environmental and health impacts of Sudan’s oil and gas industry

Namna ya kuwasilisha maombi ya ufadhili huu:

Unatakiwa kutuma maombi yako kwa kutumia Barua pepe hii; infonile2017@gmail.com

 • Andiko litakaloeleza wazo lako la habari lisilozidi ukurasa mmoja. Andiko lako linatakiwa lipangwe vyema, likieleza wazo kuu la habari yako, ambalo litafuatiwa na ni kwa namna gani, na wapi habari yako itafanyiwa utafiti. Habari hiyo inadhamiria kuibua nini au kuchangia nini, itachapishwa wapi, (chombo kipi cha habari) na matokeo tarajiwa ya habari hiyo.

Pia andiko hilo linayakiwa liwe na mpango kazi wa kuhusisha takwimu. Tafadhali zingatia kuonyesha ni kwa namna gani, utatumia media anuwai(video, picha, sauti na usanifu na maneno)

Unatakiwa pia kujumuisha:

 • Bajeti isiyozidi USD 400
 • Wasifu wako
 • Sampuli ya kazi zako zilizowahi kuchapishwa, kurushwa. Linki pekee za habari zilizochapishwa au kurushwa ndizo zinazokubaliwa. 
 • Barua ya utambulisho kutoka kwa mhariri ambaye atathibitisha kuwa chombo chako kitachapisha au kurusha  habari yako.

TAHADHARI KUHUSU COVID-19: Tutaendelea kutoa ufadhili huu, hata hivyo, tutafanya kazi na mwanahabari mmoja mmoja ili kusaidia njia salama za kuripoti wakati wa janga hili la mlipuko wa Covid-19.