Uchafuzi Jijini Khartoum: Desturi ya Kulinda Mazingira Haipo
https://www.alaraby.co.uk

Jiji la Khartoum liliinua kichwa chake, likitarajia ugonjwa wake kutibiwa kufuatia marekebisho kadhaa ya katiba…hata hivyo, hakuna kilichotendeka basi kupelekea jiji kulizika  kichwa chake tena ndani ya lindi la taka. Jiji hili kuu la Sudan, ambalo hadi mwaka wa 1950, lilikuwa jiji safi zaidi miongoni mwa majiji kuu ya Afrika limegeuka kuwa mojawapo ya jiji chafu zaidi ulimwenguni. Wataalamu wadokeza kuwa wanachokitazama sasa ni matokeo ya uwiano mbovu kati ya vitengo vidogo vidogo vya kitaifa, maeneo ya manispaa na wakubwa wao. Manispaa zilianzisha mfumo wa makampuni ya uzoaji taka, lakini zimemudu tu kuchukuwa kodi.