Rwanda: Kufurushwa kwa Wawekezaji Kutoka Kwa Vinamasi Kwafanikiwa, Ila Mengi Bado Yahitajika Kufanywa
Rwanda has over 910 wetlands that cover over 392,400 hectares.

Makala haya yameandaliwa kwa hisani ya InfoNile na Code for Africa

Na Leonce Muvuni

Serikali ya Rwanda inajitahidi kuwaondoa wawekezaji wote pamoja na kuharamisha shughuli zote zilizo kinyume na sheria ndani ya vinamasi, kwa madhumuni ya kurejesha hali yao ya kiekolojia.

Shughuli hii ya kufutilia mbali ujenzi wa aina yote kutoka sehemu zilizotengwa za vinamasi, imefua dafu kutokana na jitihada za serikali, licha ya upungufu wa hela ambayo imelegeza zoezi hili. Wizara ya Mazingira imesema kuwa juhudi hizi zinalenga kuharamisha utekeleshaji wowote uliyo kinyume na sheria ndani ya vinamasi pamoja na kufunika migodi yote iliyo kwisha kazi.

“Hivi karibuni tumeandikia tena wilaya zote na kuzihimiza kuanzisha zoezi la kurejesha hali ya vinamasi, kuanza na kufunika migodi yote iliyokwisha kazi,” alisema Vincent Biruta, Waziri wa Mazingira.

Serikali mwaka jana, ilianzisha zoezi la kuondolea mbali shughuli zote ndani ya vinamasi pamoja na zile za ujenzi, licha ya shinikizo kubwa kutoka kwa ukulima mbovu, uchimbaji haramu wa migodi na uchafuzi, utupaji taka kiholela, shughuli za ujenzi na miundo misingi iliyo haramu.

Kulingana na maagenti wanaolinda mazingira, zoezi lilitendeka wakati uharibifu wa mazingira ulisababishwa na shughuli za ujenzi ndani ya vinamasi, hivyo kufuja raslimali ya maji.

“Ukulima unaofanyika ndani ya vinamasi uharibu mimea, hivyo kupelekea udongo kushikamana hata kutoweza kuhifadhi maji, na basi kuadhiri bioanuai,” alisema Remy Norbert Duhuze, mkurugenzi katika idara inayohusika na udhibiti wa mazingara na uchafuzi ya Rwanda.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za serikali, idadi ya vinamasi nchini Rwanda ni 910 ambazo zinakalia eneo la hektari 392,400; hata hivyo, hali ya nusu ya vinamasi hivi, vinahatarishwa na uharibifu wa kiekolojia unaotokana na kilimo kibovu, kuingiliwa na shughuli za kijamii na uchumi.

Takwimu zaonyesha kwamba vinamasi vinakalia asilimia 14.9 la eneo lote la nchi, ikiwemo asilimia 6.3 maeneo ya majimaji na asilimia 8.6 ya maziwa, mito na vidimbwi vya kudumu ama vile vya majira.

Shughuli za Kilimo

Tovuti ya maji nchini Rwanda yaonyesha kwamba takriban hektari 92,000 ya vinamasi nchini humo, inatumika kwa kilimo asilia.

Wakulima hupanda viazi vitamu, pamoja na mahindi kando kando mwa vinamasi.

“Kuharamisha shughuli za kilimo katika eneo la majimaji la Rugezi, imerejesha hali yake ya kiekolojia na kuongeza kiasi cha maji kinatumika na kampuni mbili za umememaji kuzalisha umeme,” alisema Bw. Duhuze, akiongeza, “eneo la majimaji la Rugezi kwa kiasi kikubwa huthibiti, huchunga na huifadhi maji yanayotiririka ndani ya maziwa ya Ruhondo na Burera, na ambayo hutumika kwa uzalishaji umeme katika makampuni ya umeme ya Ntaruka na Mukungwa, jambo ambalo halikuwezekana mwongo uliopita.”

Eneo la majimaji la Rugezi- ambalo ndilo kinamasi kubwa zaidi nchini, liloko jimbo la kaskazini –limebainishwa siku za hivi karibuni na wanamazingira kuwa mojawapo ya maeneo yaliyo na idadi kubwa ya watu. Linaenea hadi maeneo nane ya utawala ya Cyero, Ruhunde, Kivuye, Gatebe, Burera, Butaro, Gicumbi, Miyove na Nyankenke.

Jinsi ambavyo idadi ya watu invavyoongezeka ndivyo ambavyo vinamasi vinavyo pungua.

“Tulikuwa tunakuza viazi vitamu na vile vya kijisi  katika kinamasi hiki, na hali yake ya ekolojia nusura kuharibiwa. Kiasi cha maji kilipungua, kusababisha kampuni ya umeme ya Ntaruka kukosa maji kuendesha turbine,” alisema Moses Nshimiyimana, aliyekuwa mkulima katika kinamasi cha Rugezi, Wilaya ya Burera, Jimbo la Kaskazini.

Kinamasi cha Rugezi eneo lake likiwa hektari 6,000 kilitambulika hivi karibuni na shirika la Bird Life International kuwa makao ya zaidi ya aina ya ndege 43.

“Mazao katika kinamasi hiki kwa kawaida huwa mazuri. Ndiposa kukatiza shughuli za kilimo katika kinamasi cha Rugezi hakukupokelewa vyema na jamii zimeizunguka, kwa vile huwa zinategemea kilimo,” alisema Vedaste Muneza, mkaazi wa sekta ya Butaro, wilaya ya Burera.

Kulingana na wakaazi, licha ya juhudi za kulinda kinamasi cha Rugezi, wenyeji bado huingia huko kisiri ili kuwatafutia mifugo yao lisho. Amri ya kusitisha shughuli zote ndani ya kinamasi, ilifuatia onyo kutoka kwa Rais Paul Kagame kwa wanaoingilia eneo hili pamoja na maafisa wa umma waliotoa ruhusa, kwamba watakabiliwa vilivyo.

Ufurushaji

Hivyo basi, Jiji la Kigali hivi karibuni lilianzisha zoezi la kuhamisha biashara kutoka maeneo yaliyotambulika kama vinamasi. Kutokana na zoezi hili, mali isiyopungua 2,000 na iliyohusisha viwanda, majumba ya biashara na nyumba za kuishi, ilipata kuhamishwa.

Maafisa wa serikali wanasema kuwa, zoezi hili linaendelea kuwafurusha watu kutoka hektari 7,700 ya vinamasi Jijini Kigali, zoezi ambalo linakusudiwa kutekelezwa katika maeneo yote ya nchi siku zijazo. Kati ya watakaonufaika na zoezi hili ni hifadhi ya kiwanda katika bonde la Gikondo, kilichotengwa kama kinamasi.

Kinatarajiwa kurejelea hali yake ya awali ya kiekolojia, punde tu zoezi hili, ambalo lilianza mwaka wa 2013 litakapokamilika.

Utafiti wa zoezi hili la uhamishaji Jijini Kigali laonyesha kwamba shughuli nyingi bado zahitaji ufadhili wa kifedha.

Katika kipindi cha fedha cha 2018/19 serikali ilitenga Rw9.8 bilioni kwa shughuli ya kuhamisha hifadhi kiwanda, mahali ambapo serikali inakusudia kutengeza ziwa bandia

Vincent Munyeshyaka, Waziri wa Biashara na Viwanda, alisema kuwa fedha zilizotengwa kwa shughuli hii hazitoshi, kwa vile Rwf30 bilioni zinahitajika.

Kando na kuingiliwa kwa vinamasi na kilimo kibovu, vinamasi nchini vinahatarishwa na shughuli za kijamii na kiuchumi, hii ni pamoja na wazalishaji kahawa ambao kwa kawaida hurushu maji machafu ambayo hayajatibiwa kuingia katika njia za maji.

Kulingana na baadhi ya wanamazingira, zoezi hili huchafua njia za maji moja kwa moja na kwa njia zingine pia, ambazo ni vyanzo vya maji ya kunywa kwa takriban asilimia 16 ya idadi ya wanoishi mashambani kando na kilimo cha unyunyuziaji maji kwa wakulima wadogo nchi nzima. ya awali