Ripoti ya Umoja wa Mataifa Yahimiza Hatua Dhidi ya Uchafuzi wa Kikemikali Kadiri Uzalishaji Wake Ukitarajiwa Kuongezeka Maradufu Kufikia Mwaka wa 2030
There is an urgent need for [us] to work more closely together to address the critical threats to environmental sustainability and climate – which are the foundations for life on this planet. Photo by Emmy Muchunguzi

Mataifa yatakosa kutimiza malengo yaliyokubalika ulimwenguni ya kupunguza athari za kemikali na uchafu kufikia mwaka wa 2020, hivyo kuhitajika kwa hatua za dharura ili kupunguza athari dhidi ya afya na chumi, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo.