Miongo ya Matumizi Busara Yazalisha Matunda Katika Kinamasi cha Kabale
Farmers tending to their crops in the Mugandu-Buramba wetland, where they have built their livelihoods through growing and selling Irish potatoes, beans and maize.

Makubaliano ya umiliki wa kijamii katika kinamasi cha Mugandu-Buramba kimethibiti Kinamasi hiki kwa miaka 40, huku kikiwasaidia wakulima kupata maishilio

 

Makala na midia-anuai na Fredrick Mugira

Usaidizi wa kifundi na Annika McGinnis na Code for Africa

 

Maua inachanuka katika kinamasi cha Mugandu-Buramba kusini magharibi mwa Wilaya ya Kabale nchini Uganda, kuna yale ya urujuani; meupe; mekundu; samawati na waridi – mengi yao yakiwa na umbo la bomba, yaliyomo miongoni mwa majani ya kijani kibichi.

Kinamasi cha Mugandu-Buramba, kinachotiririka ndani ya Ziwa Bunyonyi, ziwa lililo na kina cha pili kirefu Afrika, ni mojawapo ya vinamasi vingali imara nchini Uganda, nchi ambayo vinamasi vyake vingi vimeharibiwa.