Matumaini Yasitishwa Huku Gugu Likisakama Hekta 1,400 Ziwani Victoria Ndani ya Siku Nne
A view of Kisumu port on January 17. The port has become inactive as the water hyacinth continues to wreak havoc. [Denish Ochieng, Standard]

Gugu maji Ziwani Victoria limeenea kwa hekta 1,441 ndani ya siku nne, kwa mujibu wa picha za setaliti zilizotolewa na shirika la serikali hapo jana. Picha hizo zilizotolewa na taasisi ya Kenya Marine and Fisheries Research Institute (KMFRI) zilionyesha kuwa sehemu iliyofunikwa na gugu, iliongezeka kutoka hekta 6,142 mnamo February 11 na kufikia hekta 7,583 tarehe February 15.