Kuzungumza kwa Ueneaji Jangwa

“Kila mtu anipiga vita. Wanafikiri kuwa mimi ni mmbaya. Hawaelewi jinsi ninavyotamani kutulia.” Nchi inayokumbana na ukame na mafuriko. Hali ya joto nchini Sudan inakadiriwa kupanda kwa kiasi cha kati ya 1.10C na 3.10C kufikia mwaka wa 2060 hivyo, kuwa vigumu mno kuepuka madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi yanayosabavishwa na kuenea kwa jangwa. Tumealikwa kurejelea changamoto zinazotokana na kuenea kwa jangwa, kwa hali iliyotofauti, katika hadithi inayosimuliwa na jangwa lenyewe.