Bara Afrika Lazama katika Njaa Zaidi
Copyright: Panos

[DAR ES SALAAM] Inawalazimu viongozi wa Afrika kuwa na utashi wa kisiasa ili kupambana na ukosefu wa chakula kama ambavyo ripoti mpya inavyo onyesha, kwamba njaa inazidi kuongezeka kufuaitia miaka mingi ya kuzorota barani, mtaalamu amesema. Kulingana na ripoti hiyo ambayo ilizinduliwa mwezi huu (Februari 13) nchini Uhabeshi, Kusini mwa Jangwa la Sahara ndio eneo ambalo limeadhirika pakubwa, hivyo basi kulegeza juhudi za kuafikia lile lengo endelevu la pili, yaani Sustainable Development Goal 2, ambalo linalenga “kumaliza aina yote ya njaa na utapiamlo kufikia mwaka wa 2030”.