Kenya Yaangalia Ndani mwa Kisichofahamika: Hifadhi Yake ya Maji ya Chini Kwa Chini
A borehole rig drills a new water well at Shilole Primary School in Kwale, Kenya, May 23, 2018. Thomson Reuters Foundation/Isaiah Esipisu

Na Isaiah Esipisu

UKUNDA, Kenya, Julai 2 (Thomson Reuters Foundation) – Bahari zimeremetazo na kuramba upwani Diani, zimeifanya pembe hii ya kusini mashariki mwa Kenya kuwa mojawapo ya vivutio vikubwa kwa watalii.

Hata hivyo, ni wageni wachache wanaofahamu kwamba maji miferejini mwao inatoka visimani vilivyozamishwa ndani ya matabaka – hifadhi ya chini kwa chini ya maji matamu yanayotumiwa pia na wenyeji, mabiashara na kilimo.