Ziwa Cheleleka Laelekea Kukauka

Lilikuwa eneo lilotajika kuwa kiini cha mapumziko ukitumia mashua za kawaida ama motaboti na lilionyesha mandhari ya kuvutia inayotumika kutembea kando mwa ziwa. Lakini sasa asilimia 80 ya ardhi iliyokuwa sehemu ya ziwa imeshakauka na inatumika katika ukulima. Hususa kaskazini na mashariki mwa sehemu ya ziwa, shughuli kubwa ya kilimo inaendelea. Pia kuna maeneo ya ulishaji mifugo huru.