Uchungu Wa Jamii za Green Park Baada ya Kuwekeza Katika  Manyumba
One of the houses at Green Park Estate in Athi River, earmarked for demolition, on Monday, 18 2018. Read more at: https://www.standardmedia.co.ke/article/2001284612/pain-of-green-park-families-who-have-to-move-after-sinking-savings-in-houses

Francis Opiyo, mwenye umri wa miaka sitini na tisa, alitaka tu kumiliki nyumba ambayo angestaafia ndani yake, baada ya kuhudumu kama Kamanda Mkuu wa polisi wa Nyando. Alitumia marupurupu yake ya kustaafu kununua nyumba katika mtaa wa kifahari wa Green Park, hapo Athi River kwa milioni sita. Huo ulikuwa mwaka wa 2006.

Lakini huenda ndoto yake ya kuishi kwa amani miaka yake iliyosalia kuzimwa ndani ya masaa 48 ijayo. Nyumba yake ni mojapo ya zile zilizotajwa na mamlaka ya raslimali ya maji, yaani Water Resources Authority (WRA) kuwa zahitaji kubomolewa kufikia Alhamisi.

“Nilisikia kwa mara ya kwanza kuhusu uwezekano wa ubomoaji wa nyumba nikiwa mashambani kule Migori, baada ya rafiki yangu kunipigia simu na kunieleza kuwa WRA imetaja majengo kadhaa,” aeleza.

Mshtuko wa Maisha

Aliporejea kwa nyumba yake ya Green Park na kuthibitisha kuwa nyumba yake ni mojawapo ya nyumba zilizotajwa kwa ubomoaji, alizimia.