Mabadiliko ya tabia nchi yanazidisha machafuko Afrika

Mwendo usio mrefu kutoka mji wa kihistoria wa Timbuktu, Kidan, ambaye ni mzalishaji mifugo, bibi na binti yake, wanaishi kwa amani huku wamejitenga kutoka mji uliodhibitiwa na kundi haramu. Hata hivyo, kujitenga huku kunatamatika pindi mvuvi anamuuwa mmoja wa ng’ombe wake, aliyeharibu wavu wa kuvua samaki, alipokuwa akinywa maji kutoka Mto Niger. Kidan anaharakisha ili amkabili mvuvi huyo na kumfunza funzo kuhusu haki ya kila mmoja kutumia maji. Makabiliano haya yanatamatika kwa kifo cha mvuvi, hivyo kuwaweka mashakani mfugaji na jamii yake.