WATANO WAUWAWA KUTOKANA NA MAFURIKO, TANA RIVER
Locals use canoes to cross floods that cut off the road at Hamdaruku area in Tana River County. [Photo by Maarufu Mohamed/Standard]

Visa vya vifo kutokana na mafuriko maeneo ya  Kaunti ya Tana River yameongezeka kufikia tano, baada ya siku tatu ya mvua kubwa kunyesha. Jana asubuhi hapo Bilbil, kwenye barabara kuu la Bura-Garissa, mto wa msimu unaotiririka kwenye mto wa Tana, uliwasukuma watoto wawili waliokuwa wakiogelea katika mfereji ulioko katika Bura Irrigation Scheme. Watoto hao wenye umri wa kati ya miaka minane na kumi na miwili wasemekana kuzama baada ya mfereji huo kupasua kingo zake.

Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho na ambaye alijitambulisha kwa jina la Bonaya alisimulia vile wavulana hao walivyosukumwa walipokuwa wakicheza ndani ya mfereji huo, eneo la Bilbil. Mkuu wa polisi hapo Tana Kaskazini, Tom Okoth pamoja na meneja wa shirika la Kenya Red Cross anayesimamia Kaunti za Tana na Kitui, Bwana Jareld Bombe, walidhibitisha vifo hivyo. Bwana Okoth alisema timu ya maafisa wa polisi waliwekwa palipotendeka kisa hicho kutathmini hali na kulinda maisha na mali.